Advertisements

Thursday, January 27, 2022

WAZIRI KIJAJI AKUTANA NA WAWEKEZAJI NA WAMILIKI WA VIWANDA MBALIMBALI NCHINI

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt, Ashatu Kijaji, amekutana na wawekezaji, na wamiliki wa viwanda mbalimbali na kujadiili changamoto wanazokabiliana nazo na kuahidi kuzitafutia ufumbuzi kwa pamoja ili kutimiza lengo la Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini na kujenga uchumi shindani na viwanda.

Katika mikutano hiyo, Waziri Kijaji amekutana na Viongozi wa Kampuni ya Dangote Tanzania inayozalisha Saruji, Kampuni ya Coca – Cola Kwanza ltd inayozalisha bidhaa mbalimbali za vinywaji baridi na Wawekezaji wa Kampuni ya Gynile kutoka Misri inayotarajia kuanzisha kiwanda cha kuzalisha mbolea nchini.

Wakati huo huo, Waziri Kijaji amekutana na baadhi ya Watendaji na Wakuu wa Tume ya Ushindani (FFC), Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB ) na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) zilizo chini ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kujadili utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hizo katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara ili kuleta maendeleo kwa taifa.

Aidha Waziri Dkt. kijaji amezitaka taasisi zote chini ya Wizara Uwekezaji Viwanda na Biashara kufanya kazi kwa ushirikikiano na kuepuka kuwa kikwazo kwa wawekezaji, wenye viwanda na wafanyabiashara ili kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini ili kuendeleza na kukuza sekta ya uwekezaji, Viwanda na Biashara.

No comments: