Advertisements

Monday, July 4, 2022

TIMU YA KIKAPU YA JWTZ YAAGWA RASMI KUELEKEA UJERUMANI

 Wachezaji wa timu teule ya Mpira wa Kikapu ya jeshi la Ulinzi wa wananchi wa Tanzania wameagwa rasmi katika viwanja vya Don Bosco (Oyster bay) Jijini Dar es salaam kuelekea Nchini Ujerumani katika Mashindano ya Majeshi duniani.

Timu Teule ya Mpira wa Kikapu  Ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania  imeagwa rasmi Jana  Katika Viwanjani Vya Don Bosco( Oysterbey) Jijini Dar es salaam kuelekea Nchini Ujerumani  katika Mashindano Ya Majeshi Duniani ya Wachezaji watatu watatu.
Akizungumza  katika Hafla hiyo katibu wa Chama Cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (DABA )Mpoki Mwakipake amesema Familia ya Kikapu inawataakia heri katika Mashindano hayo kwa kuwa inawakilisha Mkoa Jeshi na Taifa kwa Ujumla.
" Hawa Ni Wachezaji wanatoka kwenye Ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam Ni fahari Jeshi Kuona wanayo sifa ya kushiriki Mashindano hayo"

Kwa Upande wake  Meneja wa timu hiyo Kapteni  Mohamed Kasui  alisema maandalizi yamekamilika kwa asili mia moja huku wakiahidi kurudi na Ushindi.

Alisema Mashindano hayo  ya Wachezaji watatu watatu Three On Three World Championship  yatakishirikisha  Nchi Takribani 26 zikiwemo za
Bara la Ulaya, Asia na Afrika.

Timu hiyo inajumuisha Wachezaji kumi wakiwemo Wanawake na Wanaume Viongozi.

alitaja Wachezaji hao kuwa ni Kocha Sajini Taji  Haleluya Kavalambi
Sajini Faraja Malack
Koplo Mpala Sadick
Koplo Baraka  Athumani
Koplo Penina  Lushinge
Private Mosez Jackson
Private  Selina  Msingwa
Private  Enerico Maengela na Private Alinani  Msongole.

Kwa Upande wa Manahodha wa Timu zote Mbili Faraja Malaki nahodha Wanawake na Baraka Sadick Nahodha Wanaume kwa Nyakati tofauti wameahidi kujituma na kutafuta Ushindi.

Mashindano Hayo Yatakayofanyika kuanzia Tarehe 03 Hadi 10 Julai,2022 Nchini Ujerumani Huku Timu  Kutoka Marekani,Ufaransa,Saudi Arabia,Moroco Kushiriki Mashindano hayo  Ya kidunia Ya Three On Three World Championship.

No comments: