Advertisements

Sunday, May 28, 2023

WASANII WA TANZANIA WAWA KIVUTIO MAONESHO YA MAADHIMISHO YA SIKU YA AFRIKA HUKO AFRIKA KUSINI


Na Eleuteri Mangi, WUSM, Johannesburg Afrika Kusini

Kikundi cha Ngoma na Sarakasi cha Safi kutoka jijini Dar es Salaam kimekuwa kivutio katika viunga vya jiji la Johannesburg Afrika Kusini kwa kutia fora kwa kutoa burudani safi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afrika Mei 25, 2023 na wakati wa sherehe ya Mabalozi ya miaka 60 ya Umoja wa Afrika tangu kuasisiwa kwake iliyofanyika Mei 27, 2023 Johannesburg Afrika Kusini.
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu anasema “Kikundi hiki kimependwa sana na watazamaji wakati wote, nilimuona Mhe. Rais Cyril Ramaphosa akirekodi kwa simu yake muda wote wakati kikundi hiki kinaonesha sarakasi pamoja na ngoma huku wakiwa wamependeza kwa mavazi yao ya kitanzania”.
Ziara hiyo ni utekelezaji wa wa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ambayo aliyatoa mwezi Machi 2023 wakati wa ziara yake rasmi ya kikazi nchini humo na imekuwa na faida ya kuuza utamaduni wa Tanzania katika mataifa mbalimbali ya Afrika yalihudhuria maadhimisho ya Siku ya Afrika ambayo yanawakilishwa na Mabalozi takriban 40 wanaowakilisha nchi zao Afrika Kusini na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi wa nchi hiyo.

Aidha, hafla hiyo ya Mabalozi imehudhuriwa na viongozi wa Tanzania wakiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi. Fatma Hamad Rajab pamoja na viongozi wengine kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.


TUMEJIFUNZA NAMNA YA KUTUNZA HISTORIA KUPITIA SANAA

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amesema katika ziara yao ya kikazi mji wa Century, Cape Town Afrika Kusini Mei 27, 2023 wamejifunza namna ya kutunza historia kupitia Sanaa.

“Sanamu hizi zinauwezo wa kudumu kwa muda mrefu zaidi na kuwa kumbukumbu nzuri kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo na kuwafanya waonje na kujua nchi yao imetoka wapi, ipo wapi na wanakwenda wapi hatua ambayo inatoa fundisho na kutumia historia hiyo kuinua maisha ya watu na uchumi wa nchi” amesema Bw. Yakubu
Katika ziara hiyo, yupo pia Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Bi Fatma Hamad Rajab ambao wamefika “The Long March to Freedom” kujifunza namna sanamu za shaba zinavyosadifu maisha mashujaa wa kupigania uhuru kila mmoja kwa aina yake na hazipatikani sehemu nyingine zaidi ya mji wa Century City huko Cape Town Afrika Kusini.

Miongoni mwa sanamu za kumbukumbu za mashujaa hao ipo pia ya Baba wa Taifa la Tanzania Mwl. Julius Kambarage Nyerere (1922-1999) akiwa ameorodheshwa namba kumi na mbili (12) karibu na sanamu ya namba 11 ya Helen Suzman (1917-2009) na kwa upande mwingine ipo sanamu ya namba 13 ya Fidel Castro namba (1926-1916) na viongozi wengine ambao huvuta hisia za watu wanaofika kutembelea eneo hilo ambalo ni adhimu ya ukombozi wa nchi za Afrika.



Sanamu nyingine ambazo zipo katika makumbusho hayo ni ya Walter Sisulu (1912-2003), Nelson Mandela (1918-2013), Samora Machel (1933-1986), Oliver Tambo (1917-1993), Solomon Mahlangu (1956-1979), Mohandas “Mahatma-Gandhi (1869-1948), Dkt. Martine Luther King JR (1929-1968), Archbishop Emeritus Desmond Tutu (1931-2021) pamoja na wengine wengi.



No comments: