Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi klabu ya Simba Salim Abdallah 'Try Again' amefichua mikakati ya Simba kuelekea msimu ujao
Baada ya Simba kukosa mataji kwa misimu miwili mfululizo 'Try Again' amesema unyonge huo hautakuwepo msimu ujao, wamejipanha kushinda kila mashindano watakayoshiriki
"Tunaleta wachezaji bora wenye hadhi ya kuichezea klabu ya Simba ambao tunaamini wataweza kutusaidia kutimiza malengo yetu katika mashindano ya ndani na yale ya CAF kwa kuanzia 'Super League' na ligi ya Mabingwa," alisema Try Again
Simba inaendelea kufanya usajili wa maana ambapo inaelezwa kuwa tayari imeonyesha nia ya kumnasa kiungo Milton Karisa (27) anayekipiga katika klabu ya Vipers Fc ya Uganda
Kiungo huyo ambaye amewahi kufanya kazi na kocha mkuu wa Simba Robertinho Olivieira ikiwa dili lake litajibu atakuwa miongoni mwa nyota watakaokutana na watani zao wa Jadi Yanga kwenye mechi za ushindani
Yuko kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda, 'The Cranes' kinachofanya maandalizi ya mechi za kufuzu Afcon 2023
Nyota huyo bado ana mkataba wa mwaka mmoja na timu yake hivyo mabosi wa Simba wanapiga hesabu za kuvunga mkataba wa kiungo huyo..
No comments:
Post a Comment