ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 20, 2023

FILAMU YA KISAYANSI YA EONII KUZINDULIWA JUNE 23 DAR


Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
AZAM Media Ltd (AML) na Studio za PowerBrush (PBS) wanatarajia kufanya Uzinduzi wa Filamu ya Kisayansi ya EONII Juni 23, 2023 Jijini Dar es Salaam

Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Azam Media, Divisheni ya Maudhui na Utangazaji Yahya Mohamed amesema mipango yote muhimu muhimu imekamilika tayari kwa uzinduzi huo.

“Onyesho hili la kwanza la uzinduzi wa kihistoria utafanyika Ijumaa, Juni 23, 2023 kwenye Ukumbi Century Sinemax Mlimani City Dar es Salaam, ambapo tunategemea kuwa na onyesho Maalum kwa wageni waalikwa wakipata fursa ya kushuhudia Filamu hii,” amesema Mohamed na kuongeza,

“Tutumie fursa hii kwa niaba ya Azam Media Ltd na PowerBrush Studios kutambua Mchango makubwa wa Serikali yetu katika kusimamia michezo na sanaa nchini na kuweka mipango endelevu ambayo tunashuhudia matunda yake kupitia mageuzi haya kwenye tasnia ya Filamu nchini,”.

Mohamed amebainisha kuwa Bodi ya Filamu wamekuwa mhimili mkubwa katika kutoa hamasa, kuratibu njia sahihi za kuisukuma sanaa ya Filamu na kipekee amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka chachu iliyopeleka saa sasa ya Filamu Kimataifa.

Kwamba kufuatia hamasa hizo na sera na kanuni madhubuti timu yao ya uzalishaji pamoja na PowerBrush Studios wamewekeza katika ubunifu na umakini mkubwa kunadaa Filamu ya EONII ambayo inasukuma mipaka ya kuwaza na kusimulia hadithi.

Amesema juhudi hizo za kipekee ni uthibitisho wa kukua kwa vipaji na matamanio ndani ya Tasnia ya Filamu Tanzania.

“Nimatarajio yetu viongozi na waalikwa wengine watakuwa mabalozi Wazuri baada ya onyesho la Awali la Premier siku ya Ijumaa Juni 23, 2023 pale Mlimani City, mabali na onyesho kuu la Dar es Salaam, EONII itaoneshwa katika mikoa ya Dodoma, Arusha, Tanga na Mwanza kwa upande wa Tanzania Bara, huku Zanzibar ikiwa kituo muhimu,” ameeleza Mohamed.

No comments: