Advertisements

Saturday, June 3, 2023

KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI DAR WAPEWA GARI JIPYA KWAAJILI YA KAZI MBALIMBALI ZA USALAMA BARABARANI

 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP. MULIRO J. MULIRO amesema tafsiri ya maendeleo ya kiusalama yanapimwa kwa namna ambavyo watu wanaliami na kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kulisaidia Jeshi hilo kufanya kazi kwa weledi.

SACP. Muliro ameyasema hayo leo Juni 2, 2023 wakati Kamati ya usalama barabarani ya Kanda ya Dar es Salaam ikikabidhiwa gari jipya aina ya Toyota Hilux-Revo lenye thamani ya Tsh Milioni 90 kutoka kampuni ya Motisun group litakalotumiwa na kikosi cha Usalama barabarani  Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwaajili na kazi mbalimbali za usalama barabarani.

Akiongea kwa niaba ya kampuni ya MOTISUN GROUP, Bwana PRITESH KHIMJI amesema kampuni ya MOTISUN GROUP imeamua kutoa msaada huo baada ya kuridhika na hali ya usalama iliyopo |Jijini Dar es salaam ili kuunga mkono jitihada zinafanyika katika kudumisha usalama huo.

No comments: