Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakiwasili katika Kijiji cha Ngofila Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kuhudhuria Mazishi ya Godfrid Ibenzi Ng’wele ambaye ni Baba Mzazi wa Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dkt. Ernest Ibenzi. Tarehe 20 Juni 2023.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiweka Saini katika cha maombolezo ya kifo cha Godfrid Ibenzi Ng’wele ambaye ni Baba Mzazi wa Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dkt. Ernest Ibenzi wakati alipowasili kushiriki msiba huo katika Kijiji cha Ngofila Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga tarehe 20 Juni 2023. (kushoto ni mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakishiriki Ibada ya kuaga mwili wa marehemu Godfrid Ibenzi Ng’wele ambaye ni Baba Mzazi wa Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dkt. Ernest Ibenzi iliofanyika katika Kijiji cha Ngofila Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga tarehe 20 Juni 2023. (wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na waombolezaji waliojitokeza katika Ibada ya kuaga mwili wa marehemu Godfrid Ibenzi Ng’wele ambaye ni Baba Mzazi wa Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dkt. Ernest Ibenzi iliofanyika katika Kijiji cha Ngofila Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga leo tarehe 20 Juni 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakiwafariji wafiwa mara baada ya kumalizika kwa Ibada ya kuaga mwili wa marehemu Godfrid Ibenzi Ng’wele ambaye ni Baba Mzazi wa Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dkt. Ernest Ibenzi iliofanyika katika Kijiji cha Ngofila Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga tarehe 20 Juni 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Godfrid Ibenzi Ng’wele ambaye ni Baba Mzazi wa Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dkt. Ernest Ibenzi mara baada ya Ibada ya kuaga iliofanyika katika Kijiji cha Ngofila Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga tarehe 20 Juni 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa jamii hususani watumishi wa umma kuendelea kufanya kazi kwa bidii na upendo ili kuacha alama nzuri katika Taifa na dunia kwa ujumla.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati akiwafariji waombolezaji waliojitokeza katika Ibada ya kuaga mwili wa marehemu Godfrid Ibenzi Ng’wele ambaye ni Baba Mzazi wa Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dkt. Ernest Ibenzi iliofanyika katika Kijiji cha Ngofila Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga tarehe 20 Juni 2023.
Amesema ni vema vijana na wale wote waliojaaliwa kuwa na wazazi kuona wajibu wa kuwahudumia wazazi wao kwa upendo na ukarimu mkubwa.
Aidha Makamu wa Rais amewasihi wananchi wa Kijiji cha Ngofila na watanzania kwa ujumla kuendelea kufarijiana na kuwa pamoja wakati wa changamoto zikiwemo za misiba.
Makamu wa Rais amewahakikishia wananchi wa Wilaya ya Kishapu kwamba Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ina dhamira ya dhati ya kuwaletea wananchi maendeleo na kuhakikisha huduma bora za jamii zinapatikana katika maeneo yote nchini.
Ibada hiyo imehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Madaktari pamoja na wananchi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment