ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 19, 2023

MRATIBU WA MAANDAMANO DAR AINGIA MITINI, WENZAKE WADAKWA


Jeshi la Polisi limewakamata baadhi ya vijana waliojitokeza kuandamana kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Tanzania.

Hata hivyo, mratibu wa maandamano hayo, Deus Soka katika hali ya kutofahamika, hajatokea kwenye maandamano hayo yaliyopangwa kuanzia Temeke na kuishia Ikulu, jijini Dar es Salaam

Mwananchi Digital ilipomtafuta kwa simu zake zote za kiganjani, hakupatikana na katika majina ya waliokamatwa na polisi pia jina lake halikuwepo.

CHANZO - MWANANCHI

No comments: