ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 19, 2023

OLD SCHOOL REUNION WASHINGTON DC 2023: SIMBA SC (UGHAIBUNI) 4-2 YANGA SC (UGHAIBUNI)

 Tamasha la kila mwaka la Old School lilishereheshwa kwa mtanange wa kukata na shoka kati ya Simba SC (Ughaibuni) dhidi ya Yanga SC (Ughaibuni). Pambano hilo kali lilihudhuriwa na mashabiki wengi waishio katika miji ya Washington DC, Maryland, Baltimore, Virginia na sehemu nyinginezo. 

Hadi mapumziko Yanga walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-1. Kipindi cha pili Simba walikuja kwa nguvu na kasi kama nyuki na kufunga mabao 3 bila majibu. Mgeni rasmi katika mpambano huo alikuwa ni Mwambata wa Kijeshi katika Ubalozi wa Tanzania kwa nchi za Marekani na Mexico  Col. Festus Mang’wela.

Pata picha za mpambano huo kwa hisani ya blog ya Vijimambo.




No comments: