ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 20, 2023

RAIS DKT.MWINYI AKUTANA NA WAWEKEZAJI WA CZECH NA POLAND JIJINI BERLIN


BERLIN
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amekutana na wawekezaji kutoka nchi ya Jamhuri ya Czech na Poland katika ukumbi wa Hoteli ya Berlin Marriott, Ujerumani Juni 19, 2023.
Katika mazungumzo baina ya Rais Dk.Mwinyi na wawekezaji hao wamegusia fursa zinazopatikana Tanzania hususani Zanzibar ikiwemo uchumi wa buluu, ujenzi wa mahoteli, ujenzi wa viwanda, ushirikiano katika sekta ya elimu , umeme, sekta ya afya , miundombinu, kilimo, teknolojia ya uchumi wa kijani, usafiri wa anga, mawasiliano , uwekezaji wa nyumba za makaazi kwa bei nafuu na usanifu wa majengo.
Rais Dk.Mwinyi amewakaribisha wawekezaji hao Tanzania kuangalia fursa mbalimbali za uwekezaji na kibiashara. Vilevile wawekezaji hao wamemuahidi Rais Dk.Mwinyi wako tayari kufika Zanzibar kwa ajili ya kuwekeza katika maeneo watakayokubaliana kushirikiana pande zote mbili.
Chanzo: Ikulu, Zanzibar.






No comments: