Raisa Said, Lushoto
Wilaya ya Lushoto leo imepokea mtambo wa kuchimba visima ambao utachimba visima vya maji katika maeneo kadhaa ya wilaya hiyo ambayo hayana vyanzo vya maji ya mserereko au mtiririko..
Akizungumza mjini Lushoto leo, Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini, (RUWASA), wilaya ya Lushoto,Mhandisi Erwin Senziga alisema kuwa kati ya vijiji 208 vilivyoko wilayani Lushoto, vijiji zaidi 18 havina vyanzo vya maji vya mserereko kutokana na uharibifu wa mazingira, vyanzo vya maji au mabadiliko ya tabia ya nchi.
“Mitambo hiyo inakwenda kuanza kazi katika maeneo hayo ambayo hayana vyanzo vya maji vya mserereko,” alisema Senziga.
Akielezea uletaji wa mitambo, alisema kuwa unatokana na ahadi iiyotolewa na Naibu Waziri wa Maji, Bi Maryprisca Mahundi aliyetembelea wilaya hiyo wiki iliyopita na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa, Ustaadh Rajab Abdulrahman Abdallah ambaye pia alitembelea wilaya hiyo na kuona tatizo hilo.
Mhandisi Senziga alisema kuwa wataaalmu kutoka Mamlaka ya Bonde la Mto Pangani walikwishapita katika maeneo kupima na kuainisha maeneo yanayoweza kuchimbwa na kupatikana maji hivyo alisema kuwa utekelezaji wa kazi hiyo unakwenda kuanza mara moja katika juhudi alizosema ni za kumtua mama ndoo kichwani.
Alitaja maeneo ambayo mitambo hiyo itakwenda kufanya kazi kuwa ni pamoja na sehemu za kata ya Kwekanga, Mlola na Gare.
Hata hivyo, alisisitiza juu ya wananchi kujiandaa kuchangia uednelezaji wammiradi hiyo. Alisema mitambo ikishachimba visima watatumia umeme kuyasukuma maji kkwa ajili ya matumizi hayo hivyo wananchi wakumbuke kuna kuchangia ili kuifanya miradi hiyo ya maji iwe endelevu.
“Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya mssaada huo wa mitambao ambao utafanya shida ya maji kaktika maeneo gahayo kuwa historia,” alisema.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka RUWASA, wananchi wanaopata huduma ya maji wanakadiriwa kuwa 355,021 kati ya 492,441 sawa na asilimia 72.1
wilaya ina vijiji 208 ambapo vijiji 144 vinapata huduma ya maji na vijiji 64 bado havijafikiwa na huduma ya maji.
Taarifa hyyo imetaja maeneo ambayo yanatakiwa kufanyiwa upimaji kwa ajili ya uchimbaji wa visima virefu kuwa ni kata ya Makanya yenye vijiji sita ambavyo ni Mdando,Kweulasi, Bombo, Mavului,Kwetango na Bwaya. Vijiji vingine ni Mlola, kwai, Kwemakame,, Kwekanga,Makolena Malindi.
Taarifa imesemakuwa miradi hiyoitaghraimu Sh Bilioni 10.34 na ikikamilika itanufaisha wakazi 85,655 wanaoishi maeneo mbalimbali ya wilaya ya Lushoto sawa na asilimia 17.4 ya wakazi wote wa wilaya ya Lushoto.
Imeelezwa pia hadi kufikia Septemba mwaka jana wilaya ilikwisha pokea fedha kiasi cha Sh Bilion 2.44.
“Miradi hiii ikikamilika itaongeza kiasi cha uoatikanaji wa maji kutoka asilimia 72.1 hadi kufikia asilimia 89.5,” ilisema taarifa.
No comments:
Post a Comment