ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 17, 2024

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AKUTANA NA KIONGOZI WA KAMPUNI YA YARA


MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango, ameihakikishia Kampuni ya Kimataifa ya YARA, kwamba Serikali itaendelea kuiunga mkono katika kufanya shughuli zake nchini Tanzania.

Mhe. Dkt. Mpango ametoa hakikisho hilo wakati alipokutana na Rais wa kampuni hiyo, ambaye pia ndiye Mkurugenzi Mkuu Bw. Svein Tore Holsether, kando ya Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum 2024) mjini Davos nchini Uswisi.
Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Naibu Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El Maamry Mwamba, pamoja na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Ofisi za Umoja wa Mataifa- Geneva, Mhe. Balozi Dkt. Abdallah Possi.
“Ni dhamira ya Serikali ya kuendelea kujizatiti katika uzalishaji wa mazao na kuifanya nchi kuwa ghala la chakula kikanda kwa kuzingatia ongezeko la watu pamoja na mahitaji ya chakula.” Dkt. Mpango alisisitiza.

No comments: