Friday, January 19, 2024

WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA WAZIRI WA UHAMIAJI WA BAHAMAS

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe January Makamba, amekutana na Waziri wa Uhamiaji na Bima ya Taifa wa Bahamas, Mhe. Alfred M. Sears pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) unaoendeles jijini Kampala, Uganda.

Katika kikao hicho, Viongozi hao wamesisitiza umuhimu wa nchi zao kuchukua hatua za haraka kuanzisha ushirikiano rasmi kwa ajili ya manufaa ya pande zote mbili.

Maeneo ya ushirikiano yatakayopewa kipaumbele ni pamoja na kukuza sekta ya utalii, biashara na Uwekezaji, michezo na utamaduni.

No comments: