Wednesday, February 14, 2024

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZAZIBAR OTHMAN MASOUD ATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA HAYATI EDWARD LOWASSA


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Othman Masoud Othman, Februari 13, 2024, amejumuika pamoja na Viongozi wa Serikali, Dini na Wanasiasa Mashuhuri, Viongozi Wastaafu, Mabalozi na Wanadiplomasia, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Familia na Wananchi, katika Hafla ya Kuuaga Mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa.
Hafla hiyo ambayo imefanyika katika Viwanja vya Karimjee, imeongozwa na Mgeni Rasmi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Philip Mpango.
Katika hafla hiyo, Mheshimiwa Othman ameambatana na Mke wake, Mama Zainab Kombo Shaib.

Kitengo cha Habari
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Februari 13, 2024.





No comments: