Wednesday, February 14, 2024

TUMUENZI HAYATI EDWARD LOWASSA KWA UZALENDO NA UWAJIBIKAJI WAKE - DKT. MWINYI


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema namna bora ya kumuenzi Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa ni kuendelea kuyaishi maono yake ya uzalendo, uwajibikaji ili iwe dira ya kuzidi kujenga umoja na kupiga hatua za maendeleo nchini.
Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipotoa salamu za pole na kutoa heshima za mwisho kwa Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam tarehe:13 Februari 2024.
Aidha, Rais Dk.Mwinyi ametoa salamu za Pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan na wananchi wote kwa msiba huu.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa amejifunza mengi kutoka kwa Hayati Edward Ngoyai Lowassa ukiwemo uzalendo, uwajibikaji, ushirikiano na watu wa makundi yote na kuweka mbele maslahi ya nchi.









No comments: