Raia wa Austria Rudi Stangl (62) mwenye miwani (katikati) akiwa na waongoza watalii mara baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro kwa mara 150 akifanya kazi ya kupandisha wageni kwa muda wa miaka 30 .
Raia wa Austria Rudi Stangl (62) akiwa njiani kuelekea kilele cha Uhuru Mlima Kilimajaro
Mhifadhi Vitus Mgaya kutoka idara ya Utalii (KINAPA) akimpongeza na kumvisha medali Rudi Stangl mara baada ya kushuka kutoka kilele cha Uhuru alipopanda kwa mara ya 150 .
Na Dixon Busagaga- Kilimanjaro
RAIA wa Austria Rudi Stangl (62) amejiwekea rekodi ya kupanda na kufika kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro mara 150 akifanya kazi ya kupandisha wageni kwa muda wa miaka 30 ,rekodi aliyoanza kuitafuta tangu mwaka 1982 .
Huenda Rudi akawa raia wa kwanza kutoka nchi ya Austria kuingia kwenye vitabu vya kumbukumbu vya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa kuweka rekodi hii lakini pia kuwa miongobi mwa mawakala wa utalii waliotangaza vyema kivutio cha utalii cha mlima Kilimanjaro.
Akizungumza mara baada ya kushuka lango la Marangu ,Stangl alisema kwa mara ya kwanza anapanda Mlima Kilimanjaro ilikuwa ni mwaka 1982 akiwa na miaka 21 akikumbuka maumivu aliyopata kutokana na kazi zote wakati wa safari ya kupanda alizifanya mwenyewe .
“Mara ya kwanza kupanda mlima Kilimanjaro niliumia sana kwa sababu nilibeba kila kitu mwenyewe na nilijipikia mwenyewe na nilikuwa na tembea haraka sana ,hii ni kutokana na kwamba nilikuwa vizuri sana kwenye michezo ila ilikuwa ngumu kufika Uhuru Peak ilikuwa tabu kwangu kufika pale” alisema Stangl.
Alisema baada ya miaka 12 alikuja kwa mara nyingine na kundi dogo la wageni ambao ni marafiki zake kutoka kijijini kwao na baada ya hapo ndipo akanza kufanya biashara ya kupandisha wageni Mlima Kilimanjaro kutoka nchini kwao na sasa ametimiza miaka 30 akipanda mara ya 150.
“Kwa sasa Tanzania ni kama nyumbani kwangu kwa pili na mlima Kilimanjaro ni mlima wangu pendwa niliopanda mara nyingi zaidi kuliko mlima mwingine hata kule kwetu Australia kama Kilimanjaro” alisema Stangl .
Stangl alisema watu wengi wamekuwa wakishangaa anawezaje kupanda mlima Kilimanjaro mara zote hizi na kwamba majibu yake yamekuwa ni kwa sababu anawapenda Watanzania,analipenda taifa la Tanzania lakini pia uoto wa asili uliopo Mlima Kilimanjaro.
“Huku napenda taifa hili na penda nature ya mlima ni amazing unajua mlima Kilimanjaro una kila kitu una hali zote unaanza kupanda mlima kwennye eneo la nchi kavu (dry area) unaenda hadi kwenye theluji,Hakuna mlima wowote dunia wenye nature kama hii ya mlima Kilimanjaro ,ni eneo langu pendwa nimefika mara nyingi na penda mlima kilimanjro” alisema Stangl.
Akizungumzia tofauti iliyopo sasa katka Hifadhi ya Kilimanjaro akilinganisha na mwaka 1982 wakati anapanda kwa mara ya kwanza Stangl alisema kwa sasa ameshuhudia uwepo wa nyumba nyingi za kupumzika kwa wapandaji pamoja na vyoo pamoja na umeme.
“Nature asili ya maeneo ya mlima imebadilika hili ndio kubwa zaidi theluji imepungua kwa miaka 10 iliyopita kulikuwa na theluji nyingi kuliko sasa ,3700mts kwa sasa kuna joto zamani kulikuwa na barafu kila mahali ninapo amka asubuhi sijaona hili kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita sasa” alisema Stangl .
Alisema Serikali kupitia mamlaka husika zinapaswa kufanya kitu sasa na kwamba bado kuna nafasi ya kufanya jambo zuri zaidi kwa sababu ya watalii wengi wanakuja na kwamba Kilimanjaro itakuwa sehemu nzuri zaidi kwa miaka 30 ijayo.
Kuhusu kuweka rekodi ya kupanda mara 150 katika kilele cha Uhuru ,Stangl alisema imekuwa ni Fahari kwake kutimiza azma hiyo huku akitaka ulimwengu kutambua kuhusu Kilimanjaro na kila mtu aje apande mlima Kilimanjaro .
Shirika la Hiifadhi za Taifa (TANAPA) kupitia Mhifadhi Vitus Mgaya kutoka idara ya Utalii (KINAPA) limepongeza jitihada zinazofanywa na Stangl katika kutangaza Hifadhi ya Taifa ya Kilimamanjaro kwa kuendelea kupandisha wageni kutoka nchi mbalimbali kiwemo ya Austria.
“Mr Rudi ambaye ni kiongozi wa wageni “Tour Leader” amekuwa akifanya kazi ya kuleta wageni na kuwapoandisha katika kilele cha Mlima Kilimanjaro kwa miaka 30 alianza kazi hii 1982 na leo ametimiza miaka 30 ya kazi hii na ni mara yake ya 150 kufika katika kilele cha mlima Kilimanajro.” Alisema Mgaya.
“Tunampongeza na kuwatia moyo watu wengine au viongozi wengine wanaoleta wageni waweke rekodi zao vizuri kwa kupanda mara 100 zaidi ya idadi aliyofanya Mr RudI tunampongeza sana” aliongeza Mgaya.
Mgaya alisema kama Hifadhi ya taifa ya Kilimanjaro wanaonelea kuwa hili ni jambo jema na amekuwa balozi mzuri ambaye amekuwa akitoa ushauri pindi anaposhuka kutoka mlimani akieleza nini vya kurekebisha na mawazo yake yamekuwa yakifanyiwa kazi .
No comments:
Post a Comment