Thursday, February 22, 2024

WAZIRI KAIRUKI AZINDUA VITENDEA KAZI VYA DORIA MISITUNI


Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizindua vitendea kazi vya doria misituni vyenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 6, ambavyo ni baiskeli na magari katika hafla iliyofanyika ofisi ndogo za Wizara ya Maliasili na Utalii , jengo la Mpingo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akipokea taarifa kutoka kwa Katibu wa Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF), Dkt. Tuli Msuya kuhusu magari mawili yaliyokabidhiwa kwa Wakala ya Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa ajili ya kusaidia jitihada za Wakala hiyo katika kujenga uwezo wa kusimamia misitu kwa ufanisi, katika hafla iliyofanyika ofisi ndogo za Wizara ya Maliasili na Utalii , jengo la Mpingo.
Baadhi ya baiskeli zilizokabidhiwa kwa Wakala ya Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (hayupo pichani) kwa ajili ya kusaidia kazi za doria misituni katika hafla iliyofanyika ofisi ndogo za Wizara ya Maliasili na Utalii , jengo la Mpingo leo Februari 20,2024 jijini Dar es Salaam.

Magari yaliyokabidhiwa kwa Wakala ya Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (hayupo pichani) kwa ajili ya kusaidia kazi za doria misituni katika hafla iliyofanyika ofisi ndogo za Wizara ya Maliasili na Utalii , jengo la Mpingo leo Februari 20,2024 jijini Dar es Salaam.

No comments: