Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje akizungumza kuhusu kazi zinazofanywa na chuo hicho wakati wa kufunga kozi za Viashiria vinavyoweza kuleta hatari kwenye viwanja vya ndege(Best Practice in Risk Management) na Utamaduni wa Kiusalama(Security Culture) kwa siku tano kwa wakaguzi wa Usafiri wa Anga kutoka nchini Tanzania na Somalia zilizofanyika katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) kwa kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa kushirikiana na Tume ya Usafiri wa Anga ya Ulaya(ECAC).
Mkufunzi kutoka ECAC Charlote Lund akizungumzia mchango wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa kushirikiana na Tume ya Usafiri wa Anga ya Ulaya(ECAC) na Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) walivyoweza kuedesha kozi ya kuwajengea Uwezo wa Kiukaguzi ya siku tano kwa wakaguzi wa Usafiri wa Anga kutoka nchini Tanzania na Somalia.
Baadhi ya wakaguzi wa Usafiri wa Anga kutoka nchini Tanzania na Somalia, wakufunzi kutoka Tume ya Usafiri wa Anga ya Ulaya (ECAC) wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje alipokuwa anafunga mafunzo hayo.
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje (wa pili kushoto) akitoa vyeti kwa washiriki wa kozi ya kuwajengea Uwezo wa Kiukaguzi ya siku tano kwa wakaguzi wa Usafiri wa Anga kutoka nchini Tanzania na Somalia iliyofanyika katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) kwa karatibiwa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa kushirikiana na Tume ya Usafiri wa Anga ya Ulaya(ECAC).
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC), wakufunzi kutoka Tume ya Usafiri wa Anga ya Ulaya (ECAC) na wakaguzi wa Usafiri wa Anga kutoka nchini Tanzania na Somalia mara baada ya kufunga kozi za Viashiria vinavyoweza kuleta hatari kwenye viwanja vya ndege(Best Practice in Risk Management) na Utamaduni wa Kiusalama(Security Culture) kwa siku tano kwa wakaguzi wa Usafiri wa Anga.
Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya(EU) kimeendesha kozi za Viashiria vinavyoweza kuleta hatari kwenye viwanja vya ndege(Best Practice in Risk Management) na Utamaduni wa Ki usalama(Security Culture) kwa siku tano kwa wakaguzi wa Usafiri wa Anga kutoka nchini Tanzania na Somalia.
Kozi hizo zilizoandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Somalia (SCAA) na kudhaminiwa na Umoja wa Ulaya (EU), imefungwa na Mkuu wa Chuo cha CATC Aristid Kanje.
Kozi hizo mbili zilikuwa za nadharia na vitendo katika uwanja wa ndege ambapo washiriki na idadi yao katika mabano kutoka Somalia-SCAA(6) , TCAA na CATC(7), Mamlaka ya Viwanja vya ndege -TAA(2), Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro -KIA(2), Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar-ZAA(2) .Wengine ni Travel Control(2), Uwanja wa ndege wa Dodoma (1), Uwanja wa Ndege Arusha(1), na Jeshi la Polisi (2).
Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa awamu mbili yalikuwa kama ifuatavyo Kozi ya Viashiria vinavyoweza kuleta hatari kwenye Viwanja vya ndege Februari 26-28, 2024, ilikuwa na jumla ya washiriki 12 ( sita kutoka Tanzania na sita kutoka Somalia)na Kozi ya Utamaduni wa Ki usalama Februari 29,2024 mpaka Machi 1,2024 ilikuwa na washiriki 25(19 kutoka Tanzania na Sita kutoka Somalia).
Awali Mkufunzi kutoka EU Charlote Lund aliishukuru CATC kwa kuratibu mafunzo hayo kwa ufanisi katika kipindi chote cha mafunzo na kuwapongeza washiriki wa kozi kwa kuonyesha ushirikiano wa hali ya juu licha kuwa wametoka mataifa tofauti.
CATC ni moja katika vyuo vya mafunzo ya ICAO upande wa Usalama wa Usafiri wa Anga(ASTC).
No comments:
Post a Comment