Advertisements

Friday, April 19, 2024

RAIS SAMIA NA MWENYEJI WAKE RAIS ERDOGAN WA UTURUKI WASHUHUDIA MIKATABA IKISAINIWA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais Recep Tayyip Erdoğan wakishuhudia Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. January Makamba na Rais wa Baraza la Elimu wa Uturuki Dkt. Erol Ozvar wakitia saini Makubaliano ya Ushirikiano katika Nyanja ya Elimu ya Juu baina ya nchi hizo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais Recep Tayyip Erdoğan katika picha ya pamoja na mwakilishi wa Tanzania ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji TIC Bw. Gilead Teri na mwakilishi wa Uturuki ambaye ni Makamu wa Rais wa Ofisi ya Rais Uwekezaji ya Jamhuri ya Uturuki Zeynel Kilınç, mara baada ya utiaji saini Hati za makubaliano baina ya mataifa hayo mawili tarehe 18 Aprili, 2024
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais Recep Tayyip Erdoğan wakati wakishuhudia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Lela Muhamed Mussa pamoja na Rais wa Baraza la Utalii la Uturuki Abdullah Eren wakisaini hati za makubaliano kwa ajili ya kuanzisha ufadhili kwa wanafunzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Uturuki wanaohitimu katika Elimu ya Juu tarehe 18 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Ziara yake Rasmi katika Ikulu Kulliye Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.
Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdoğan akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Ikulu Kulliye Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.

No comments: