Thursday, May 23, 2024

AJALI YAUWA WATU 11 KIWANDA CHA SUKARI MTIBWA

 
Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda Sukari cha Mtibwa Sugar, Bw. Seif Ali Seif , akiwa na uso uliojawa na huzuni kwenye eneo la tukio
WATU 11 wakiwemo raia watatu wa kigeni wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa na kukimbizwa hospitali ya Misheni ya Bwagala kwa matibabu baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme katika kiwanda cha Sukari cha Mtibwa wilayani Mvomero mkoani Morogoro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Alex Mkama, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya saa 8 kuelekea saa 9 usiku na kusababisha vifo hivyo.
“Ni kweli tukio hilo limesababisha vifo vya watu 11 na majeruhi wawili, wengi walikjuwa ni wataalamu ambao walikuwa kazini tangu jana jioni na hadi muda huo walikuwa wanaendelea na kazi ya kufanya maandalizi ya uzalishaji.” Amesema Kamanda Mkama

Aidha Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokozi Mkoa wa Morogoro, Shaban Marugujo amewaambia waandishi wa habari kwenye eneo la tukio kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni bomba la kusafirisha gesi kiwandani hapo kupasuka na kusababisha mlipuko wa moto ambao uliwaunguza watu 13 kati yao 11 wamepoteza maisha huku wengine wawili wakijeruhiwa.

No comments: