Saturday, May 18, 2024

WAZIRI SIMBACHAWENE AMEWATAKA WAHITIMU WA MAFUNZO YA UONGOZI KUWA MFANO BORA KWA JAMII


l
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na wahitimu wa Stashahada ya Uzamili ya Uongozi, Programu ya Uongozi kwa Wanawake na Programu ya Uongozi ngazi ya Cheti wakati wa mahafali ya saba ya Taasisi ya Uongozi yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed Said akihimiza uwajibikaji kwa Wahitimu wa Stashahada ya Uzamili ya Uongozi, Programu ya Uongozi kwa Wanawake na Programu ya Uongozi ngazi ya Cheti wakati wa mahafali ya saba ya Taasisi ya UONGOZI yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu-IKULU, Bw. Mululi Majula Mahendeka akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na Wahitimu wa Stashahada ya Uzamili ya Uongozi, Programu ya Uongozi kwa Wanawake na Programu ya Uongozi ngazi ya Cheti wakati wa mahafali ya saba ya Taasisi ya UONGOZI yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Bw. Kadari Singo akielezea maudhui ya mafunzo yanayotolewa na taasisi yake wakati mahafali ya saba ya Taasisi ya UONGOZI ya wahitimu wa Stashahada ya Uzamili ya Uongozi, Programu ya Uongozi kwa Wanawake na Programu ya Uongozi ngazi ya Cheti yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya UONGOZI wakifuatilia mahafali ya saba ya Taasisi ya UONGOZI ya wahitimu wa Stashahada ya Uzamili ya Uongozi, Programu ya Uongozi kwa Wanawake na Programu ya Uongozi ngazi ya Cheti yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wahitimu wa Stashahada ya Uzamili ya Uongozi, Programu ya Uongozi kwa Wanawake na Programu ya Uongozi ngazi ya Cheti wakionesha vyeti walivyotunukiwa na Mgeni rasmi Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani) wakati wa mahafali ya saba ya Taasisi ya UONGOZI yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wahitimu wa Stashahada ya Uzamili ya Uongozi, Programu ya Uongozi kwa Wanawake na Programu ya Uongozi ngazi ya Cheti wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene alipokuwa akizungumza nao wakati wa mahafali ya saba ya Taasisi ya UONGOZI yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wahitimu wa Stashahada ya Uzamili ya Uongozi, Programu ya Uongozi kwa Wanawake na Programu ya Uongozi ngazi ya Cheti wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene alipokuwa akizungumza nao wakati wa mahafali ya saba ya Taasisi ya UONGOZI yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene amewataka Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi kuwa mfano katika jamii na kutumia taaluma waliyoipata kwa kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, uwazi na haki.

Mhe. Simbachawene ameyasema hayo leo tarehe 17 Mei,2024 katika Ukumbi wa Mliman City Jijini Dar es Salaam wakati wa mahafali ya saba ya wahitimu wa mafunzo ya uongozi yanayotolewa na Taasisi ya UONGOZI kwa kushirikiana na Chuo cha Aalto EE cha Nchini Finland.

“Mafunzo ya uongozi yanathamani kubwa sana, hivyo, tunataka kuona uongozi wa kimkakati wenye manufaa zaidi katika usimamizi wa rasilimaliwatu na fedha, tunataka kuona mnaboresha nyanja ya mawasiliano na mahusiano baina yenu na wadau wengine wa masuala ya maendeleo ndani na nje ya nchi” amesisitiza Mhe. Simbachawene.

Mhe. Simbachawene ameongeza kuwa Kiongozi mzuri ni yule anayewajibika na kuhakikisha anaacha alama, kwa mantiki hiyo hategemei kuona wahitimu hao wanakwenda kufanya kazi kwa mazoea bali watatumia uwezo wao na elimu waliyoipata kuleta matokeo chanya kwa ustawi kwa jamii.

Kwa upande wake, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Jakaya Kikwete amewataka wahitimu hao kuwa chachu na kuleta mapinduzi katika maeneo yao ya kazi huku akiwasisitiza kuendelea kusoma zaidi kwa manufaa yao na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

“Kutokana na taarifa ya mafunzo mliyopata, mimi binafsi sitarajii kusikia wala kuona mnaendekeza tabia ya kutumia simu muda wa kazi wakati wananchi wanasubiri huduma na majibu ya changamoto zinazowakabili” alisema Mhe. Kikwete.

Aidha, Mhe. Kikwete ameto rai kwa wahitimu hao kutambua kuwa dhima kubwa ya uongozi ni kuonesha njia sahihi kwa wengine ili kuleta maendeleo ya haraka na yenye ufanisi.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Taasisi ya UONGOZI, Bw. Kadari Singo amesema, Taasisi hiyo ina jukumu kubwa la kuandaa na kuendesha mafunzo kwa viongozi, kuendesha majadiliano ya kisera na kufanya tafiti za kisera, kutoa ushauri wa kitalaam na kuzisaidia taasisi mbalimbali pamoja na viongozi wake katika kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Taasisi ya UONGOZI (UONGOZI INSTITUTE) ilianzishwa Julai, 2010 kwa malengo ya kuwa na kituo cha utalaam wa juu cha kuendeleza viongozi Barani Afrika kwa kuanzia nchini Tanzania, Kanda za Afrika Mashariki na hatimaye Afrika nzima.

Katika Mahafali hayo ya saba ya Taasisi ya UONGOZI, jumla ya wahitimu 198 wamefuzu na kutunukiwa vyeti wakiwemo Watumishi wa Umma na Sekta binafsi katika Astashahada ya Uzamili katika Uongozi, Mafunzo ya Uongozi ngazi ya Cheti, na Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake.

No comments: