Sunday, May 19, 2024

MWENGE WA UHURU WAWASILI WILAYA YA MJINI UNGUJA


Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B Hamida Mussa Khamis kushoto akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Mjini Rashid Simai Msaraka ili kuutembeza katika Wilaya yake hafla iliofanyika Mazizini kambi ya Jeshi Zanzibar.
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Makwaya Joseph Makwaya akipimwa Suti wakati walipofika kuuangalia Mradi wa Vijana (Suti Zanzibar Kampun Ltd)Mchina Getini Ikiwa ni katika kutembelea Miradi mbalimbali Wilaya ya Mjini Zanzibar.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Godfrey Mzava akipatiwa maelezo na Mkurugenzi wa Suti Kampuni Ltd Ali Mohamed Ali wakati alipotembelea Mradi wa Kampuni hio katika mbio za Mwenge wa Uhuru ili kujuwa maendeleo na Changamoto za Vijana hafla iliofanyika Mchina Getini Zanizbar.
Katibu wa Idara ya UeneziItikadi na Mafunzo CCM Khamis Mbeto Khamis akiupokea Mwenge wa Uhuru baada ya kuwasili katika Ofisi za CCM Kisiwandui Zanzibar.
Wakimbiza Mwenge wa Uhuru wakiwa wamejipanga katika Kaburi la aliekua Rais wa Kwanza wa Zanzibarmarehemu Mzee Abeid Amani Karume wakati walipofika katika Ofisi za CCM Kisiwandui Zanzibar.
Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru Godfrey Mzava akieka Shada la Maua katika kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Sheikh Amani Abeid Karume wakati alipokwenda kumuombea Dua Kisiwandui Zanzibar.
Mkuu wa Wilaya ya Mjini Rashid Simai Msaraka akizungumza baada ya kuwasili Mwenge wa Uhuru katika Ofisi za CCM Kisiwanduzi Zanzibar.
Wakimbiza Mwenge wa Uhuru wakiukimbiza katika eneo la michenzani kuelekea Kisiwandui katika ofisi za CCM ili kwenda kumuombea Dua Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Zanzibar.

Na Imani Mtumwa
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa 2024 Godfrey Eliakimu amewataka wananchi kushiriki katika matembezi ya mbio za mwenge ili kutekeleza miradi mbalimbali iliopangwa. Ameyasema hayo huko katika Kiwanja kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wa makabidhiano ya mwenge wa uhuru 2024 kutoka Wilaya ya Magharibi B na kukabidhiwa wilaya ya Mjini.

Mzava ameushukuru uongozi wilaya ya magharibi B na Wananchi kwa ujumla kwa mashirikino mazuri waliofanya wakati mwenge wa uhuru ukiwa katika wilaya hiyo jambo ambalo limepelekea mwenge huo kutembezwa kwa vizuri katika maeneo yaliopangwa.

Amesema lengo la mbio za mwenge huo ni kuangalia Maendeleo ya miradi mbali mbali inayotekelezwa sambamba na kujuwa Fedha zilizotumika katika kuimarisha Nchi.

Akizungumza katika zoezi la upandaji wa miti huko kilimani Plaza, kiongozi huyo amewataka viongozi na wananchi kujenga utamaduni wa kupanda miti kwani ni muhimu kwa kuepusha majanga, kuzuia mmongonyoko wa ardhi na kuhifadhi mazingira kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Mjini Rashid Simai Msaraka amesema Serikali imeweka mikakati mbali mbali ya kuengeza upandaji wa miti ili kuhakikisha wilaya ya mjini inakua na kivutio cha misitu hapa Zanzibar.

“Malengo ya Serikali kupitia mradi huu ni kuhakikisha tunaimarisha mji wa Zanzibar kuwa katika mazingira mazuri na kufikia dhamira ya kuwa kivutio cha Utalii.” alisema Msaraka.

Vile vile amesema kuna miradi mingi ya upandaji miti ili kuepusha majanga yanayoweza kujitokeza ingawa tatizo kubwa ni uelewa mdogo kwa baadhi ya wananchi katika suala la upandaji wa miti.

Jumla ya miradi Nane imetembelewa na kuwekewa jiwe la msingi katika wilaya ya mjini ikiwemo upandaji wa miti kilimani plaza, mradi wa Vijana Mpendae, ujenzi wa maduka skuli ya darajani, kutembelea kituo cha mabasi kijangwani na mradi wa maji safi na salama Saateni ambapo ujumbe wa mbio za mwenge mwaka huu ni "umuhimu wa kuhifadhi mazingira na kutunza vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na uchumi wa taifa".

No comments: