Monday, July 22, 2024

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MADARASA SHULE YA BENJAMIN MKAPA SIMANJIRO


Na John Walter -Simanjiro

Mwenge wa Uhuru umezindua mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu matatu ya vyoo katika shule ya Sekondari Mererani Benjamin William Mkapa iliyopo wilaya ya Simanjiro uliogharimu shilingi milioni 61.

Taarifa ya mkuu wa wilaya ya Simanjiro Mwalimu Fakii Lulandala imeeleza kuwa nguvu za wananchi katika mradi huo ni Shilingi Milioni 5,560,500.

Mradi huo utaongeza wigo wa wanafunzi wa kidato kuingia shuleni kwa mkupuo mmoja na kuondoa msongamano wa wanafunzi darasani.

Aidha kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mnzava ameridhia kuzindua mradi huo.

Kaulimbiu, Tunza Mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa Ujenzi wa taifa endelevu.

No comments: