· Ni matunda ya ziara ya Rais Samia India
Na Mwandishi Wetu
DAKTARI bingwa wa upasuaji wa magoti na nyonga kutoka hospitali maarufu diniani YASHODA iliyoko mji wa Hyderabad nchini India, Dk. Ram Mohan Reddy na wenzake, wanatarajiwa kuwasili nchini mwezi huu kwaajili kutoa matibabu ya upasuaji wa kibingwa wa magoti na nyonga.
Madaktari hao watafanya upasuaji huo kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa upasuaji wa magoti na nyonga wazawa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili- tawi la Mloganzila ambapo matibabu hayo ya kibigwa yatafanyika.
Mkurugenzi mtendaji wa Global Medicare, ambao ni mawakala wa tiba utalii nchini, Abdulmalik Mollel, alisema madaktari hao watafanya upasuaji wakibigwa katika hopitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila kuanzia tarehe 26 hadi 28 mwezi huu.
Mollel alisema madaktari hao bobezi watashirikiana na madaktari bingwa wazawa kwenye kambi hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo madakitari wa ndani kwa kubadirisha uzoefu ambao utawapa ujunzi zaidi madaktari wenyeji ambao utawawezesha kufanya upasuaji kama huo hata baada ya kuondoka kwa daktari huyo mgeni.
“Mwaka jana tulifanya kambi kama hii ya upasuaji na ilikuwa na mafanikio makubwa sana kwasababu kulikuwa na watu zaidi ya 2,300 waliokuwa wanahitaji huduma hiyo na madaktari wetu walifanya kazi kubwa sana kwa kushirikiana na wale wa nje na tunatarajia daktarin huyu bingwa na bobezi na wenzake katika matibabu ya upasuaji wa nyonga na magoti watawafanyia watu wengi watakao jitokeza mapema nakufanyiwa uchunguzi wa awali,” alisema
Alisema baada ya uchunguzi wale watakao ngundulika wanahitaji matibabu hayo ya kibigwa ya upasuwaji watafanyiwa.
Alisema kwa muda mrefu watanzania wenye matatizo ya afya walikuwa wakienda nje ya nchi kwa matibabu lakini baada ya serikali kuwekeza kwa kiasi kikubwa kwenye sekta ya afya watanzania wengi wamekuwa wakitibiwa hapa hapa nchini.
Mollel alisema serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye vifaa tiba kwa kuzingatia teknolojia ya kisasa kama iliyoko kwenye mataifa makubwa duniani na imesomesha wataalamu bobezi ( super specialist) wa fani mbalimbali kwenye tiba.
“Tanzania kwa sasa inavifaa vya kisasa vya kutosha na wataalamu bobezi kama walioko nchini India na kwinginemko kwa hiyo sasa ni muda mwafaka madaktaari bobezi wa nje waje hapa nchini kujengeana uwezo (Capacity building) na wenzao wa ndani ambao wamekuwa wakifanyakazi kubwa sana kwaajiri ya Taifa,” alisema Mollel ambaye pia ni Mkurugenzi wa Global Education Link (GEL).
Alisema huduma za madaktari wabobezi zinazopatikana hapa nchini zimewavutia watu wengi wa nchi jirani kuja kutibiwa hapa nchini badala ya kwenda nchi za nje kufuata tiba kama hiyo ambapo hutumia muda mwingi na gharama kubwa kulinganisha na kuja hapa nchini.
“Kuja kwa madakatri hawa wabobezi ni jambo jema sana kwasababu madaktari wetu watachukua zile teknolojia ambazo zitakuwa hazijafika hapa nchini nasisi kama tuna ujuzi ambao tumewazidi wanachukua na kwa uwekezaji uliofanywa na serikali katika sekta ya afya Tanzania sasa ni kitovu cha utalii tiba kwa nchi za Afrika Mashariki na kusini mwa jangwa la sahara,” alisema Mollel.
“YASHODA ni miongoni mwa hospitali kubwa duniani inayopatikana nchini India yenye vitanda 4,000 kwa hiyo inafanya vizuri sana na mwaka jana mwezi wa tano ujumbe wa madaktari bingwa wa Tanzania walienda kujifunza wao wanakitu gani tofauti na hivi tulivyonavyo, tulijifunza wanamazingira gani yanayosababisha watu duniani kupendelea kwenda kutibiwa kwao,” alisema
Aidha, alisema lengo lilikuwa ni kujifunza yale ambayo yamewafanya wawe bingwa kwenye utalii tiba duniani na kuja kutekeleza nchini yale ambayo wameyafanya yakawapa sifa ya kuwa kitovu cha utalii tiba na kupata wagonjwa kutoka mataifa mbalimbali duniani.
“Moja ya mafanikio ya ziara tuliyofanya India mwaka jana ni ujio wa madaktari kutoka YASHODA ambayo ni moja ya hospitali tulizotembelea zenye ubora na viwango vya daraja la kwanza duniani na ina madaktari mahiri na wenye mtandao mkubwa duniani kutokana na ubobezi wao,” alisema
No comments:
Post a Comment