Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile akizungumza na uongozi wa uongozi wa Kampuni ya Uwakala wa Meli ya Nyota Tanzania LTD (MAERSK Tanzania) alipofanya ziara ya kukagua na kusikiliza changamoto za katika Kampuni hiyo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Nelson Mlali alipofika katika Kampuni ya Uwakala wa Meli ya Nyota Tanzania LTD (MAERSK Tanzania) katika ziara ya kukagua na kusikiliza changamoto za Bandari kavu ya Bravo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Fedha Kampuni ya Nyota Jimmy Kabwelle kuhusu kazi zinazofanywa na Kampuni ya Uwakala wa Meli ya Nyota Tanzania LTD (MAERSK Tanzania) katika ziara ya kukagua na kusikiliza changamoto za Bandari kavu ya Bravo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile akutana na kuzungumza na Viongozi Makampuni ya Uwakala wa Meli ya Nyota Tanzania LTD (MAERSK Tanzania) na Sturrock Flex Shipping LTD jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yake ametumia fursa hiyo kuwaeleza kuhusu maboresho mbalimbali yanayofanywa na Serikali katika Miundombinu ya Bandari ikiwemo Dar es Salaam, Tanga, Mtwara na Bandari za Maziwa nchini, Ukarabati na Ujenzi wa Meli, Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR na maboresho katıka reli ya Kati na kuwasisitiza kutumia fursa hiyo kwa kuendelea kushawishi mashirika Mengi zaidi kutumia Bandari ya Dar es Salaam na Bandari nyingine zilizopo nchini.
Aidha, Naibu Waziri Kihenzile amewaahidi kufanyia kazı changamoto zote zilizowasilishwa ili kutokwamisha shughuli za uchukuzi nchini.
Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Nelson Mlali alipofika katika Kampuni ya Uwakala wa Meli ya Sturrock Flex Shipping LTD katika ziara ya kukagua na kusikiliza changamoto za Bandari kavu ya Bravo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile akipata maelezo kutoka kwa Hashim Ahmed kuhusu kazi zinazofanywa na Kampuni ya Uwakala wa Meli ya Sturrock Flex Shipping LTD katika ziara ya kukagua na kusikiliza changamoto za Bandari kavu ya Bravo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile akizungumza na uongozi wa uongozi wa Kampuni ya Uwakala wa Meli ya Sturrock Flex Shipping LTD alipofanya ziara ya kukagua na kusikiliza changamoto za katika Kampuni hiyo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Nelson Mlali pamoja na uongozi wa Kampuni ya Uwakala wa Meli ya Sturrock Flex Shipping LTD mara baada ya kumaliza kuzungumza na uongozi wa Kampuni hiyo.
No comments:
Post a Comment