Tuesday, August 27, 2024

SERIKALI YAZINDUA MRADI WA KUPUNGUZA GESIJOTO


Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi akizindua Mradi wa Kuandaa Mkakati wa Taifa wa muda mrefu wa kupunguza Uzalishaji wa Gesijoto jijini Dodoma Agosti 26, 2024.
Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Catherine Bamwenzaki akitoa neno la utangulizi wakati wa kikao cha uzinduzi wa Mradi wa Kuandaa Mkakati wa Taifa wa muda mrefu wa kupunguza Uzalishaji wa Gesijoto jijini Dodoma Agosti 26, 2024.
Bi. Viktoria Dimitrova kutoka Asasi ya 2050 Pathways akizungumza wakati wa kikao cha uzinduzi wa Mradi wa Kuandaa Mkakati wa Taifa wa muda mrefu wa kupunguza Uzalishaji wa Gesijoto jijini Dodoma Agosti 26, 2024.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Bw. Ilyasa Pakacha Haji akizungumza wakati wa kikao cha uzinduzi wa Mradi wa Kuandaa Mkakati wa Taifa wa muda mrefu wa kupunguza Uzalishaji wa Gesijoto jijini Dodoma Agosti 26, 2024.


Washiriki wakiwa katika kikao cha uzinduzi wa Mradi wa Kuandaa Mkakati wa Taifa wa muda mrefu wa kupunguza Uzalishaji wa Gesijoto jijini Dodoma Agosti 26, 2024.
Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kuizndua Mradi wa Kuandaa Mkakati wa Taifa wa muda mrefu wa kupunguza Uzalishaji wa Gesijoto jijini Dodoma Agosti 26, 2024.


Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imezindua Mradi wa Kuandaa Mkakati wa Taifa wa muda mrefu wa kupunguza Uzalishaji wa Gesijoto ambao utasaidia kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Mradi huo utakaotekelezwa nchini Tanzania kwa kipindi cha mwaka mmoja utasaidia kujenga uwezo wa nchi katika kukabiliana na ongezeko la joto hadi kufikia chini ya nyuzijoto 15.

Akizungumza wakati wa kikao cha uzinduzi wa mradi huo jijini Dodoma Agosti 26, 2024, Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi amesema mkakati huo unatarajiwa kuandaliwa ni muhimu kujumuisha mambo muhimu ya kitaifa.

Amewataka wadau kutoka sekta mbalimbali zinazoshiriki katika maandalizi yake kuongeza ufanisi wa nishati zinazotumiwa na jamii ambazo ni safi zisizochafua mazingira ambazo Tanzania imejiwekea lengo kuwa asilimia 80 wananchi watatumia nishati safi ifikapo mwaka 2030.

Halikadhalika, Naibu Katibu Mkuu Mitawi amesema nishati inayotumika viwandani nayo inapaswa kuangaliwa kwani inaposambaa angani husababisha ongezeko la joto ambalo ni chanzo cha mabadiliko ya tabianchi.

Ameongeza kuwa kwa vile eneo la usafiri linaweza kusadia katika kupunguza gesi joto ambalo ambapo kwa sasa tayari Serikali imeanzisha mradi wa reli ya kisasa (SGR) na mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam (DART) hivyo kuwe na mkakati wa kuitekeleza katika maeneo mengine ya nchi.

Amesema ni wakati sasa mkakati huo ujumuishe namna ya kufanya biashara ya kaboni na fursa zake pamoja na upandaji wa miti na kuitunza huku akipongeza Zanzibar kwa kuja na kampeni ya kukijanisha visiwa hivyo.

Awali akizungumza, Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Catherine Bamwenzaki amesema lengo la mradi huo kuandaa mkakati wa kukabiliana na gesijoto kulingana na kifungu cha 4 (19) cha Makubaliano ya Paris kinachotoa masharti kwa Wanachama kuunda na kuwasiliana Mikakati ya Muda Mrefu ya Uzalishaji wa Uzalishaji wa gesi chafu, kwa kuzingatia Kifungu cha 2.

Pia, amesema kikao hicho kilichowakutanisha washiriki 50 kutoka sekta mbalimbali za Serikali na binafsi kimelenga kutoa taarifa kwa wadau kuhusu namna ya kutekeleza mradi huo ulioandaliwa katika kipindi cha miaka mitatu kabla ya kuanza utekelezaji wake

Naye Bi. Viktoria Dimitrova, kutoka Asasi ya 2050 Pathways Platform amesema mbali ya Tanzania pia ni nchi zilizonufaika ni pamoja na Pakstan, Rwanda, Jamaica na Senegal.



Amesema katika utekelezaji wa miradi hii ni muhimu kushirikiana na Serikali katika kuandaa mipango madhubuti ya muda mrefu katika kukabiliana na gesijoto.



Mradi huo unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, ufadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kupitia taasisi yake ya Internation Climate Initiative (IKI) na kusimamiwa na Asasi ya 2050 Pathways Platform.

















No comments: