ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 26, 2024

TUME YAWAOMBA WADAU WA UCHAGUZI KUWA MABALOZI WAZURI


Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe.Balozi Omar Mapuri amewaomba wadau wa Uchaguzi kuwa Mabalozi wazuri wa kufikisha taarifa na kuwahamasisha wananchi kujitokeza katika kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Wito huo umetolewa na Mhe.Balozi Mapuri wakati akifunga Mkutano wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na wadau wa Uchaguzi uliofanyika mkoani Manyara tarehe 25 Agosti, 2024 ikiwa ni maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura zoezi linalotarajiwa kuanza mkoani humo tarehe 4 Setemba hadi tarehe 10 Septemba, 2024.

“Pia napenda kuwaomba wadau wa uchaguzi kwa umoja wenu, kuzingatia sheria za uchaguzi, kanuni za Uboreshaji na maelekezo ya Tume kuhusu zoezi la uboreshaji wa Daftari” alisema Mhe.Balozi Mapuri.

Aidha Mhe.Balozi Mapuri aliongeza kwa kusema kuwa hamasa kuwa ya wananchi kushiriki katika zoezi la Uboreshaji wa Daftari na baadaye uchaguzi utachangiwa kwa kiasi kikubwa sana na hamasa kutoka kwenu hivyo natoa rai kwenu muwaelimishe wananchi wanaokwenda vituoni kutojiandikisha zaidi ya mara moja.

Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura unatarajia kuanza mkoani Manyara kwa baadhi ya Halmashauri tarehe 4 Septemba hadi tarehe 10 Septemba, 2024 sambamba na mikoa ya Simiyu na Mara.


No comments: