Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele, akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza jana Agosti 26 na kumalizika leo Agosti 27, 2024 Mkoani Mkoani Mara.
Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele, akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza jana Agosti 26 na kumalizika leo Agosti 27, 2024 Mkoani Mkoani Mara.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Bw. Kailima Ramadhani, akizungumza wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza jana Agosti 26 na kumalizika leo Agosti 27, 2024 Mkoani Mkoani Mara.
Na Mwandishi wetu
Watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wametakiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura muda wote hata kama hakuna waombaji wa kujiandikisha vituoni.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele wakati akifunga mafunzo kwa watendaji wa uboreshaji ngazi ya mkoa wa Mara na halmashauri za mkoa huo.
Amesema watendaji wa vituo wanapaswa
kuwepo vituoni muda wote kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa 12 kamili
jioni kila siku katika siku saba za kujiandikisha zilizowekwa na Tume.
“Muda wa kufungua na kufunga kituo uwe
ni ule uliopangwa ili waombaji wanapohitaji kuja kituoni kujiandikisha watukute
kituoni,” amesisitiza Mhe. Mwambegele.
Tukio kama hilo la kufunga mafunzo
limefanyika pia mkoani Simiyu ambako Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi
Mhe. Magdalena Rwebangwira amewataka watendaji hao kufuatilia kwa karibu zoezi
hilo ili lifanikiwe, kutoa kipaumbele kwa makundi mbalimbali na kuwa makini
katika usambazaji na utunzaji wa vifaa.
Akifunga mafunzo ya watendaji Mkoani
Manyara, Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ambaye pia ni Jaji wa
Mahakama Kuu, Mhe. Asina Omari kwa upande wake amehimiza uhamasishaji wa wapiga
kura na kuwa Tume inatarajia wapiga kura halali tu ndio wapatiwe kadi za mpiga
kura.
“Mnahimizwa kuhamasisha wananchi wenye
sifa ili wajitokeze kujiandikisha na kupata haki yao ya kikatiba
itakayowawezesha kushiriki kuwachagua viongozi wao. Aidha ni matarajio ya Tume
kuwa baada ya zoezi hili kukamilika watu watakaopatiwa kadi watakuwa ni wapiga
kura halali,” amesema Jaji Asina.
Mafunzo haya yanafanyika ikiwa ni
maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mzunguko wa
nne unaojumuisha mkoa wa Mara, Simiyu na baadhi ya halmashauri za Mkoa wa
Manyara ambazo ni Halmashauri ya Mji wa Babati na Halmashauri za Wilaya za
Babati, Hanang na Mbulu ambapo uboreshaji utaanza tarehe 04 Septemba, 2024 hadi
10 Septemba, 2024 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na
kufungwa saa 12:00 jioni.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu Asina Omari akizungumza wakati akifunga mafunzo hayo mkoani Manyara.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo kutoka mkoa wa Manyara.
Meza Kuu wakiwa katika picha wakati wa kufunga mafunzo kwa mkoa wa Manyara.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Magdalena Rwebangira akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo kwa upande wa Mkoa wa Simiyu.
Washiriki wakisikiliza kwa makini hotuba ya kufunga mafunzo.
Washiriki kutoka Mkoa wa Simiyu wakishiriki mafunzo kwa vitendo
--
No comments:
Post a Comment