Monday, September 9, 2024

WAZIRI MHE.DKT.PINDI CHANA ATETA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA


Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete (kulia) akizungumza kuhusu ushirikiano baina ya Benki ya Dunia na Tanzania katika masuala ya uhifadhi wakati wa kikao kati yake na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) (wa pili kutoka kulia) kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) akizungumza na ujumbe kutoka Benki ya Dunia ukiongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete katika kikao kilichofanyika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete (kulia) mara baada ya kikao kati yao kilichofanyika katika kikao kilichofanyika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dodoma.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Benki ya Dunia ukiongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete katika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii, jijini Dodoma.

Ujumbe huo umekuja kumpatia mrejesho wa ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Benki ya Dunia hasa katika uhifadhi wa maliasili na utekelezaji wa mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW)ikizingatiwa kwamba Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) ameteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuiongoza Wizara hiyo.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Chana ameishukuru Benki ya Dunia kwa namna ambavyo imeendelea kuiwezesha Tanzania kwenye juhudi zake za uhifadhi na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshugulikia maliasili, Kamishna Benedict Wakulyamba na Mratibu wa Mradi wa REGROW, Aenea Saanya.

No comments: