Tuesday, October 29, 2024

MAMA MARIAM MWINYI KUSHIRIKI MKUTANO WA MERCK FOUNDATION


MKE wa Rais wa Zanzibar , Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mhe.Mama Mariam Mwinyi ameondoka Zanzibar na kuwasili Jijini Dar es Salaam.

Mama Mariam Mwinyi atashiriki Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary , utakaofanyika tarehe 29-30 Oktoba 2024 katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wageni zaidi ya 700 kutoka Mataifa mbalimbali duniani, ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mkutano huu unalenga kujadili na kutafuta suluhu dhidi ya changamoto mbalimbali za afya na kijamii zinazokabili bara la Afrika na Asia.

No comments: