ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, October 6, 2024

MKE WA PROF JAY AULA UWEKA HAZINA BAWACHA

Mke wa Prof Jay akiwa katika pozi baada ya ushindi huo.
Dar es Salaam 5 Oktoba 2024: Grace Mgonjo ambaye ni Mke wa mwanamuziki na Mbunge wa zamani Jimbo la Mikumi Chadema, Joseph Haule maarufu kama Prof Jay, leo ameula katika nafasi ya Uweka Hazina wa Baraza la Wanawake Chadema Kanda ya Pwani
Akipongezwa na wanachama wenzake, kushoto ni Rose Moshi ambaye ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa BAWACHA.
Akizungumza na Global Tv baada ya kupata ushindi huo Grace amesema anamshukuru Mwenyezi Mungu na wanawake wenzake waliomuamini kwenye nafasi hiyo na deni alilonalo sasa ni kuwatumikia wanawake hao.
Ameendelea kusema kuwa jukumu lake muhimu litakuwa ni kushirikiana na wenzake kuwasimamia vyema wanawake wa Chadema kushinda nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa vijiji na vitongoji pamoja na uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani. CHANZO HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS GLOBAL PUBLISHERS. 

No comments: