Friday, October 25, 2024

TCAA YATOA ELIMU KWA WADAU SEKTA YA UCHUKUZI


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Salim Msangi akiwasilisha taarifa ya utendaji ya TCAA katika Mkutano wa 17 wa Tathimini ya Utekelezaji katika Uchukuzi na Usafirishaji ulioandaliwa na Wizara ya Uchukuzi unaofanyika jijini Arusha kuanzia Oktoba 23- 25, 2024 katika kituo cha mikutano cha kimataifa Arusha (AICC).

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Salim Msangi amewasilisha taarifa ya utendaji ya TCAA katika Mkutano wa 17 wa Wadau wa Sekta ya Uchukuzi kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini unaofanyika jijini Arusha kuanzia Oktoba 23- 25, 2024 katika kituo cha mikutano cha kimataifa Arusha (AICC).

Mkutano huo wa siku tatu unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), ulifunguliwa na Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa umewakutanisha wakuu wa Taasisi chini ya Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Ujenzi, TAMISEMI pamoja na wadau wa sekta ya uchukuzi kutoka sekta binafsi.

Wasilisho hilo limegusa mipango ya Taasisi, mafanikio pamoja na changamoto ambapo wadau walijadili kwa pamoja namna bora ya kuboresha utendaji ili kuboresha sekta ya usafiri wa anga nchini.

TCAA inashiriki Mkutano huu ambapo inapata nafasi ya kukutana na wadau kujadili maendeleo katika sekta ya uchukuzi nchini.

No comments: