Wanajumuiya wa North Carolina wakijumuika pamoja na kutoa pole kwa familia ya Musisa baada ya kupata msiba wa mpendwa wao Mzee Ntinginya Seif Musisa aliyepatwa na umauti Octoba 1, 2024 katika taasisi ya Transitions LifeCare iliyopo Raleigh, North Carolina na mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa nyumbani Tanzania mkoani Tabora kwa maziko.
Wanajumuiya North Carolina wakijumuika pamoja na familia ya Musisa na kutoa pole walipokutana nyumbani wa marehemu Raleigh, Northa Carolina siku ya Jumamosi Octoba 5, 2024.
Wanajumuiya wakipata machopochopo baada ya kujumuika pamoja na familia ya mzee Musisa nyumbani kwa marehemu Raleigh, North Carolina.
Wanajumuiya wakijumuika pamoja na familia ya Musisa nyumbani kwa marehemu.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi
No comments:
Post a Comment