ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 7, 2024

SHERIA ZA USALAMA BARABARANI NDIO MUONGOZO WENU MKIWA MNAENDESHA VYOMBO VYA MOTO


Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Wilaya ya Ileje Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Raphael Magoma Novemba 07,2024 ametoa elimu kwa Madereva akiwa katika barabara ya Mpemba-Ileje na kuwachukukia hatua za kisheria kwa wale wote wasiozingatia sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali zinazoweza kuepukika.
Pia, Mkaguzi Magoma aliwataka abiria kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za madereva wazembe ambao wamekuwa hawafuati na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili wachukuliwe hatua za kisheria na iwe fundisho kwa madereva wengine wenye tabia kama hizo.
Sanjali na hilo, Mkaguzi Magoma, amewaasa madereva wa maguta kutoendesha kwa mwendokasi na kupakia mizigo kwa njia ya hatari kwani jiografia ya Wilaya hiyo ina mitelemko mikali na milima mingi hivyo wanaweza kusababisha ajali ambazo zinaweza kuepukika.
Mkaguzi Magoma ameendelea kutekeleza dhana ya Polisi jamii ya kutoa elimu kwa madereva na wamiliki wa vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria ili kuweza kuwakumbusha namna ya kuheshimu na kuzingatia Sheria hizo.

No comments: