Watahiniwa wa Bodi wakiendelea na mitihani
Bodi ya wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imeendesha mitihani yake ya 29 kwa jumla ya watahiniwa 1,223 katika ngazi za Professonal Diploma, Graduate Professional na CPSP. Mitihani hiyo imefanyika katika mikoa Dar es Salaam, Dodoma, Kilimanjaro, Arusha, Mbeya, Mwanza na Zanzibar kuanzia terehe 11 hadi 15 Novemba, 2024.
Akizungumza wakati wa mitihani hiyo ikiendelea, Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka Bodi ya wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Bw. Amani Ngonyani amesema ni muhimu sana kwa wahitimu kutoka vyuo mbalimbali waliosoma masomo ya Ununuzi na Ugavi na wale wanaofanya kazi za Ununuzi serikalini na sekta binafsi ila hawana sifa za kitaaluma kuja kufanya mitihani ya Bodi hiyo ili waweze kupata sifa za kitaalam za kufanya kazi za Ununuzi na Ugavi kwa ubobezi na ufanisi zaidi hili linachagizwa na uwepo wa Mtaala mpya unaowajengea watahiniwa wa PSPTB weledi na umahiri zaidi katika taaluma hiyo.
Bw. Ngonyani amesistiza zaidi kwamba waajiri wasiajiri watumishi katika eneo la ununuzi na ugavi wasiokuwa na sifa stahiki na hususani wale ambao hawajafanya mitihani ya kitaaluma na kuwa na ujuzi na maarifa stahiki.
“Bodi hii iko macho na hatua stahiki za kisheria na kimaadili zitaendelea kuchukuliwa kwa wale wanaokiuka sheria, kanuni na matakwa ya maadili ya Utendaji kazi iwe ni kwa wataalam wa fani ya Ununuzi na Ugavi au wengine wote wanafanya kazi za ununuzi na ugavi pasipo kuwa sifa kwa kuwa kujisajili na kufanya mitihani hii kumerahishwa sana, haihitaji tena mtu kuja PSPTB ila kwa kutumia simu janja yake au kompyuta yake anaweza kujisajili na kufanya mitihani hii. Aidha tayari kuna baadhi ya vituo vimeanza kutoa mafunzo ya kuwawezesha watahiniwa wa pembezoni au mbali na vituo vya kujifunzia kupata nafasi na fursa ya kusoma hivyo nahimiza wadau wote tushirikiane wakiwemo waandishi wa habari kuhakikisha kazi za Ununuzi na Ugavi zinafanywa na watu wenye sifa za kitaalam na kielimu. Alisema Bw. Ngonyani
Pia amewasisitiza waajiri wenye watumishi wanaopaswa kufanya mitihani ya kitaaluma ili kuwa sifa zinazohitajika kuwapa ruhusa watumishi hao ili waweze kujiendeleza na pia wawalipie ada za mafunzo na za mitihani ili kuwawezesha watumishi hao kufanya mitihani hii muhimu kwa mustakabali wa utendaji wenye tija katika Taasisi zao.
No comments:
Post a Comment