Na John Walter -Arusha.
Viongozi mbalimbali wa serikali, wananchi, ndugu, na jamaa wamekusanyika leo katika kata ya Olmoti, jijini Arusha, kwa ajili ya kushiriki mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe, aliyefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro (KCMC).
Mazishi hayo yamehudhuriwa na watu kutoka nyanja mbalimbali za kijamii, kiserikali, na kibiashara.
Miongoni mwa waliowasili kutoa heshima zao za mwisho ni pamoja na mfanyabiashara maarufu bilionea David Mulokozi anayemiliki Kiwanda cha kuzalisha vinywaji changamshi Mati Super Brands, Mkuu wa Wilaya ya Magu, Joshua Nassari, na aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.
Viongozi mbalimbali waliozungumza wakati wa shughuli hiyo, walitoa salamu za pole kwa familia na kuwataka waendelee kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu.
Alimtaja marehemu kama kiongozi aliyekuwa na bidii ya kazi na aliyejitolea kwa dhati kuwatumikia wananchi wa Mbozi.
Ndugu, jamaa, na marafiki walitoa ushuhuda wa maisha ya marehemu, wakimtaja kuwa mtu wa watu, mwenye upendo, na mchapakazi asiyechoka.
Mazishi haya yameacha simanzi kubwa kwa familia, wananchi wa Mbozi, Manyara alipowahi kuhudumu kama Mbunge wa viti maalum kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM na taifa kwa ujumla.
Marehemu ameacha alama kubwa katika utumishi wa umma, na mchango wake utaendelea kukumbukwa kwa muda mrefu.
Mazishi yamefanyika kwa heshima zote, huku maombi maalum yakifanyika kwa ajili ya kuiombea roho ya marehemu.'
Picha ikiwaonesha waombolezaji kwenye Mazishi hayo.
No comments:
Post a Comment