CHIFU WA MBEYA ROCKETI MASOKO MWANSHINGA AKEMEA WANAPANGA KUZUIA
WANANCHI KUJITOKEZA KWENYE UCHAGUZI
Chifu wa Mkoa wa Mbeya, Rocketi Masoko Mwanshinga, amewataka wananchi wote wa mkoa huo
kutumia haki yao ya kikatiba kujiandikisha na kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Chifu Mwanshinga amekemea vikali wale wote wanaotaka kuwazuia wananchi kushiriki katika mchakato
wa uchaguzi, akisema Mungu atawapa usingizi na hawataweza kuzuia uchaguzi kufanyika.
Amesisitiza kuwa kila raia ana haki ya kupiga kura na kupigiwa kura bila hofu wala vizuizi vyovyote. A
idha, Chifu Mwanshinga amemuombea Rais Samia Suluhu Hassan apate ushindi wa kishindo, akisema kuwa uongozi wake umekuwa wa neema kwa Watanzania.
Amewataka wakazi wa Mbeya kuungana kwa mshikamano na kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao wa kidemokrasia ili kuchagua viongozi watakaosukuma mbele maendeleo ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment