ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 30, 2026

NDANI YA DAKIKA 15 JINSI MADAKTARI BINGWA WA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI WALIVYOFUTA GIZA LA MIAKA MINGI TABORA

 


Mapinduzi makubwa ya kihistoria katika sekta ya afya yanaendelea kushuhudiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora ambapo ambapo madaktari bingwa wa macho kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda za Nyanda za Juu kusini wameweka kambi maalum ya upasuaji wa mtoto wa jicho kuwezesha kuwarejeshea nuru, utu, na tabasamu zaidi ya wananchi 400 ambao hapo awali wamekuwa gizani, huku ikivunja kuta za kijiografia na kifedha kwa familia masikini.

Wakitumia ujuzi wa hali ya juu Wataalamu hao wameweza kufanya upasuaji salama unaochukua wastani wa dakika 15 kwa kila magonjwa ambapo dakika hizi chache zimekuwa na thamani ya dhahabu, zikifuta giza la miaka mingi na kuwapa wagonjwa fursa ya pili ya kuona ulimwengu na kuzitua familia masikini mzigo mzito wa gharama za kusafiri umbali mrefu kufuata matibabu hayo ya kibingwa mkoani Mbeya au mikoa mingine ya mbali.

Akizungumza na wanahabari Daktari kiongozi wa timu ya wataalamu hao Dkt. Barnabas Mshangila wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ameeleza kuwa ugonjwa wa Mtoto wa jicho huwasababisha watu uwezo wao wa kuona wa kushiriki kwenye shughuli za kiuchumi kama kulima, kufanya biashara, na kujitegemea, jambo linaloongeza utegemezi wa kiuchumi ndani ya ngazi ya familia.

Ameeleza kuwa kambi hiyo ya matibabu ya upasuaji wa mtoto wa jicho  haijarejesha tu uwezo wa kuona, bali imempa kila mwanafamilia husika aliyekuwa akimwongoza ndugu wake fursa na uhuru wa kurejea katika shughuli binafsi au shuleni kwa Watoto katika ukombozi wa kielimu na utamaduni mpya unaookoa mustakabali wa kizazi kijacho cha wana-Sikonge

“Kwa kuwarudishia uwezo wa kuona zaidi ya wananchi 300, kambi hii imefungua milango ya kiuchumi kwa zaidi ya watu 600—ikijumuisha wagonjwa wenyewe na wauguzi wao ambao sasa wamepata uhuru. Sasa, nguvu kazi hii muhimu inarejea kwa kasi mashambani na kwenye biashara, hatua itakayochochea ukuaji wa uchumi wa wilaya ya Sikonge na kupunguza umaskini.” – Dkt. Mshangila

Nae Meneja wa Shirika la Kimataifa la Helen Keller Intl nchini Tanzania, Athuman Tawakal ameeleleza kuwa mafanikio ya kambi hii ni matokeo ya muundo thabiti wa kiuongozi na ushirikiano wa kimkakati kutoka taasisi kuu tatu, Wizara ya Afya kwa mwongozo thabiti wa kisera na uratibu wa kitaifa, ikihakikisha huduma hizi za kibingwa zinawafikia wananchi wa maeneo ya pembezoni kwa usawa na viwango vya juu zaidi, Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Nyanda za juu kusini kama moyo wa operesheni hii, kwa kuonyesha uzalendo na weledi wa hali ya juu kwa kutoa huduma bila uchovu na Shirika la Hellen Keller International nguzo kuu katika utoaji wa rasilimali, vifaa tiba, na kuhamasisha jamii ili kuondoa unyanyapaa na hofu dhidi ya upasuaji wa macho.

Zaidi ya wananchi 400 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho katika kambi hii ya siku saba, iliyoanza tarehe 25 Oktoba na inayotarajiwa kuhitimishwa rasmi tarehe 31 Oktoba,








No comments: