Didier Drogba
Mshambuliaji wa Ivory Coast Didier Drogba, kiungo wa Ghana Michael Essien na mpachika mabao wa Cameroon Samuel Eto'o wametajwa kuingia mchujo wa wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mwaka 2009.
Wachezaji hao watatu walikuwa nguzo kuziwezesha nchi zao kufuzu kucheza fainali za mashindano ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini.
Samuel Eto'o tayari ameshinda tuzo hiyo mara tatu kuanzia mwaka 2003-2005.
Drogba alishinda tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika mwaka 2006, lakini mwenzake wa Chelsea, Essien amekwishateuliwa hatua ya mchujo mara nne, lakini hajashinda hata mara moja.
Mwaka 2009 Drogba aliteuliwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka wa Afrika wa tuzo ya BBC.
Nahodha wa TP Mazembe Tresor Mputu Mabi aliteuliwa kuwa mwanasoka bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka ndani ya bara la Afrika.



No comments:
Post a Comment