
Mkuu wa jeshi la polisi nchini Algeria, Ali Tounsi, ameuawa kwa kupigwa risasi katika mji mkuu, Algiers.
Aliuawa nyakati za asubuhi wakati wa mkutano wa kawaida katika makao makuu ya polisi mbele ya maafisa wenzake.
Muuaji huyo inaaminika alikuwa ni afisa mwenzake wa polisi.
Baadae mtu huyo alijaribu kujiua lakini akajeruhiwa vibaya kwa risasi katika jaribio lake hilo na kwa sasa anashikiliwa akiwa anatibiwa hospitalini mjini Algiers.
No comments:
Post a Comment