Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amekiri Ufaransa na Jumuia ya Kimataifa walifanya makosa wakati wa mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka 1994.Lakini hakuomba msamaha kwa kina na akasema ana matumaini wote waliohusika wataadhibiwa.
Alitoa maoni yake wakati wa ziara ya kwanza ya Rais wa Ufaransa nchini Rwanda tangu yalipotokea mauaji ya kimbari.
Ziara hiyo ina lengo la kuonesha ishara ya maelewano baina ya nchi hizo mbili baada ya kipindi kirefu cha kutoelewana.
Rwanda inaituhumu Ufaransa kwa kutoa mafunzo na silaha kwa Wahutu wenye msimamo mkali, walioendesha mauaji ya Watutsi wanaofikia 800,000 pamoja na Wahutu wenye msimamo wa wastani, madai yanayokanushwa na Ufaransa.
Wakati wa ziara hiyo Bw Sarkozy akifuatana na mwenyeji wake Rais Paul Kagame alitembelea makumbusho ya watu waliouawa wakati wa mauaji ya kimbari.
Katika mkutano mkutano wa pamoja na waandishi wa habari Bw Sarkozy alielezea masikitiko yake kutokana na matukio yaliyochochea mauaji ya kimbari.
No comments:
Post a Comment