
Maelfu ya waandamanaji wa aliyekuwa waziri mkuu, Thaksin Shinawatra, wanakusanyika katika mji mkuu wa Thailand, Bangkok, wakitaka serikali ivunje bunge na kuitisha uchaguzi mpya.
Misafara ya malori na mabasi imekuwa ikiwasili katika mji mkuu ikiwa imebeba waandamanaji waliovalia shati zao za kipekee zenye rangi nyekundu.
Waandamanaji wanasema wako tayari kuendelea kubaki mjini Bangkok kwa siku kadhaa.
Lakini viongozi wa waandamanaji hao wamesema vuguvugu lao limepiga hatua katika kampeni kubwa dhidi ya kile walichosema ni kundi la watu maarufu lisilozingatia demokrasia.
Mara ya mwisho kwa waandamanaji hao kuandamana kwa idadi kubwa, mwezi April mwaka uliopita, maandamano yao yaligeuka na kuwa ghasia za barabarani.
Serikali ikikumbuka hayo, imeanza utekelezaji wa sheria za usalama wa ndani, ambazo zinaipatia jeshi la taifa uwezo maalum wa kushughulikia ghasia.
No comments:
Post a Comment