ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, March 14, 2010

Museveni asema Kony ameonekana Darfur

Joseph Kony
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kiongozi wa kundi la waasi la Lords Resistance Army, ameonekana karibu na jimbo la Darfur, magharibi mwa Sudan.
Kiongozi wa kundi hilo la waasi wa LRA, Joseph Kony, anatakikana kwa uhalifu wa kivita na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai.
Mapema wiki hii shirika linalopinga mauaji ya kimbari la "Enough" lenye makao yake mjini Washigton, lilisema kuwa vikosi vya LRA vilielekea Darfur, na kuonya kuwa vinaweza kusababisha matatizo wakati wa uchaguzi wa Sudan.
Kony amekataa kutia saini mkataba wa amani na serikali ya Uganda kwa sharti la kufitiliwa mbali kwa hati ya mahakama hiyo ya kimataifa inayoagiza kukamatwa kwake, na baadhi ya wasaidizi wake.
Kundi la LRA limekuwa likipigana na serikali ya Uganda katika miaka ishirini iliyopita na uasi huo umesababisha watu wapatao millioni mbili kukimbia makaazi yao.

No comments: