ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 22, 2010

Mgomo wa BA waingia siku ya tatu


     
Maelfu ya wasafiri British Airways wanahangaika kufuatia mgomo wa wafanyikazi wa shirika hilo kwa siku ya tatu leo.
Safari nyingi zimepangwa kurejelewa hii leo. British Airways inayoaminika kuwa shirika kubwa zaidi la ndege duniani imesema kuwa wengi wa wahudumu wa ndege wamepuuza wito wa kuendelea na mgomo kwa hivyo inaweza kurejesha safari zaidi.
Hata hivyo muungano unaowatetea wafanyikazi wanaogoma umesema kuwa bado wako imara na sasa wameitisha mkutano mwingine na shirika hilo la ndege kuzuia mgomo mkubwa wa wiki ijayo. Bado kampuni ya British Airways haijatoa jibu.

No comments: