
Mshukiwa wa ugaidi anayeaminika kuwa raia wa Somalia anayeishi Australia, ametoweka kutoka mikononi mwa polisi nchini Kenya.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, maafisa wa idara ya uhamiaji walimkamata mshukiwa huyo mapema mwezi huu katika mpaka wa Kenya na Uganda magharibi mwa nchi hiyo.
Hata hivyo, mtu huyo aliyekamatwa kwa madai ya kuwa na paspoti bandia, aliweza kutoweka kabla ya polisi wa kukabiliana na ugaidi kufika kumhoji.
Vyombo vya habari nchini Kenya vinasema kuwa mtu huyo huenda ni mwanachama wa kundi la wapiganaji wa al-Shabab nchini Somalia lenye uhusiano na kundi la kigaidi la al-Qaeda.
No comments:
Post a Comment