Bunge la waakilishi mjini Washington, Marekani limepitisha mswada wa afya wa Rais Barack Obama, mswada unaotazamiwa kuwa mkubwa zaidi katika mabadiliko yanayofanyiwa sheria za kijamii nchini humo. Kulitokea shangwe upande wa Demokrats katika bunge walipopata kura 216 zilizohitajika kupitisha mswada huo. Akimalizia kampeini za mjadala juu ya mswada huo, spika wa bunge Nancy Pelosi alisema kuwa bunge la Marekani linafikia hatua ya kihistoria. Mwandishi wa BBC mjini Washington amesema kuwa nafasi za rais Barack Obama kupata ushindi ziliongezwa baada ya kuafikiana na wanademokrats waliopinga kutumiwa fedha za hazina ya umma katika uavyaji mimba. Mjadala wa mswada huu ulipamba moto huku wanaharakati walioupinga wakifanya maandamano nje ya majengo ya bunge. | |||
ANGALIA LIVE NEWS
Monday, March 22, 2010
Mswada wa afya wa rais Barack Obama wapitishwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment