ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, March 13, 2010

Mwili wa dereva aliyefia Polisi kuchunguzwa kesho

UCHUNGUZI wa mwili wa dereva wa teksi aliyekufa mikononi mwa polisi wiki hii unatarajia kufanyika kuanzia kesho na daktari aliyechaguliwa na familia ya marehemu.

Akizungumza nyumbani kwake jana, baba wa marehemu Juma Selanda, alisema baada ya kukutana na Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alikubali uamuzi wa familia kumkataa na daktari wa serikali na kumteua dakatari wanayemuamini.


" Tulikutana na Kova na amekubaliana na wazo letu la kuwa na daktari huru wa kufanya uchunguzi, kwasababu leo (jana) na kesho (leo) sio siku ya kazi basi uchunguzi huo utafanyika muda wowote kuanzia Jumatatu (kesho),“ alisema huku akikataa kutaja jina la daktari kwa lengo la kufanya usiri.

" Hatuwezi kumtaja daktari tuliyomtafuta, ila uchunguzi wake ni muhimu kwani riporti yake tunaisubiri sisi na polisi pia na baada ya uchunguzi tutachukua maiti yetu na kwenda kuzika,“ alisema

No comments: