ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 1, 2010

Terry ajibu matamshi ya Bellamy


 Craig Bellamy
                                          John Terry
John Terry amejibu matamshi yaliyoonekana kumkera kutoka kwa Craig Bellamy wa Manchester City.
John Terry alinyoosha mkono wake kumsalimia Wayne Bridge siku ya Jumamosi, lakini Bridge akaukwepa.
Nahodha wa Chelsea John Terry amemjibu Craig Bellamy baada ya kumsema kufuatia ushindi wa Manchester City katika uwanja wa Stamford Bridge wa Chelsea.
Bellamy alifunga mabao mawili katika ushindi wa Manchester City wa mabao 4-2 siku ya Jumamosi na kumtupia vijembe nahodha wa zamani wa England kutokana na tabia yake nje ya uwanja.
Bellamy amesema"Nafahamu JT kama alivyo mtu yeyote katika soka anafahamu jinsi alivyo nje ya uwanja."
John Terry amejibu kwa kutumia nahau "Mtu anayeishi katika nyumba ya vioo asirushe mawe."
Matamshi ya Bellamy yanaonekana kuzidi kumkera nahodha wa Chelsea, ambaye katika mchezo wa Jumamosi na City alizembea na kusababisha kufungwa bao moja.

No comments: