
Nchini Uholanzi, mamia ya wanaharakati wanaounga mkono ndoa za mapenzi ya jinsia moja walitoka nje wakati misa ikiendelea katika kanisa moja la katoliki ambapo walikuwa wamekusanyika kupinga sera ya kanisa hilo juu ya uhusiano wa aina hiyo.
Walivuruga misa kwa nyimbo na kumzomea kasisi aliyekataa kumpa sakramenti mmoja wa waumini hao aliyetangaza wazi kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Uholanzi ni taifa la kwanza bara Uropa kuidhinisha ndoa za aina hiyo katika mwaka wa 2001.
Hata hivyo kanisa Katoliki nchini humo limeendelea kupinga ndoa hizo.
No comments:
Post a Comment