ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 1, 2010

Yanga hamko peke yenu,Kotoko na Orlando watoka mapema Afrika


Mabingwa wawili wa zamani wa Afrika Asante Kotoko ya Ghana na Orlando Pirates ya Afrika Kusini wametolewa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa wa bara hilo.
Mabingwa mara mbili wa Afrika, Kotoko waliifunga ASC Linguere ya Senegal kwa mabao 2-0 mjini Accra siku ya Jumapili, lakini wakatolewa baada ya mikwaju 4-2 ya penalti.
Orlando Pirates nao pia walishindwa kuvuka kikwazo cha awali baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Gaborone United ya Botswana katika uwanja wa Nelson Mandela Bay .
Orlando walikuwa wakiongoza kwa mabao 2-0 yaliyopachikwa na Katlego Mashego na Bennett Chenene.

No comments: